Harare, Zimbabwe. Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye anazuiliwa nyumbani wake mjini Harare amekutana na ujumbe wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika( Sadc), Serikali ya Afrika Kusini imesema.
Hata hivyo, hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa mbali ya kusisitizwa kuwa pande hizo zimekuwa na mazungumzo mjini Harare. “ Sadc imekuwa ikikutana na Rais Mugabe Ikulu,” alisema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini, Clayson Monyela alipozungumza na AFP.
Hayo yanajiri huku mawaziri wa mambo ya nje wa Sadc wanakutana nchini Botswana katika kikao cha dharura kilichoitishwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo ambaye pia Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma. Mugabe amekuwa akizuiliwa nyumbani wake tangu Jumatano na amekuwa akishinikizwa aachie madaraka kwa amani.
No comments:
Post a Comment