Chama hicho kimesema hakukuwa na ulazima wowote kwa Dk Mpango kueleza suala hilo bungeni kwani ni jambo binafsi kati yake na Rais Magufuli.
Hivi karibuni wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka 2018\2019, Dk Mpango alisema Rais Magufuli amewataka wabunge hao ambao michango yao imekosoa uendeshaji wamepeleke majina ya wawekezaji wanaokwamishwa ili awape kazi
Dk Mpango alisema, “Naomba ninongo’neza na Bunge lako Tukufu. Mheshimiwa Rais Magufuli aliposikia huu mjadala alinipigia na aliniambia hivi,” alisema Dk Mpango
“Waziri waambie ndugu yako mheshimiwa Bashe kuwa nawataka sana wawekezaji hao wa Standard Gauge Railway.
Lakini leo Novemba 16 ACT kupitia kwa kaimu mwenyekiti wake, Yeremia Maganja kimeibuka na kusema “Dk Mpango ni yeye ni waziri na haya mambo binafsi kati yake na Rais Magufuli na hakulazimika kuyaweka bungeni. Maana yake Dk Mpango anataka kutuonyesha Rais Magufuli ni ofisa ugavi ambaye ana uwezo wa kuelekeza miradi badala ya Bunge.
“Ndiyo maana tunasema Dk Mpango amekuwa mpango kweli, wewe unaongea na Rais unakuja kuwaambia watu? Rais angetaka angeongea na Spika.
No comments:
Post a Comment