Jeshi la Zimbabwe Robert Mugabe anawasiliana na aliyekuwa msaidizi wake Emmerson Mnangagwa, ambaye alifukuzwa kazi takriban wiki mbili zilizopita, hali iliyosababisha jeshi kuongoza nchi.
Jeshi hilo limesema Bwana Mnangagwa atarejea nchini humo katika siku za karibuni na kutangaza kuwa wanafanya kazi na Rais Mugabe kukubaliana jinsi ya kutatua tatizo linaloikabili nchi hiyo.
Chama tawala cha Zanu PF ambacho kinataka Bwana Mnangagwa kuchukua nafasi ya Rais Mugabe, Jumanne kinatarajia kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais.
Afisa Mwandamizi wa chama hicho Paul Mangwana anasema Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93 anatuhumiwa kumpa madaraka makubwa mke wake, Grace, hali ambayo ni ukiukwaji wa katiba ya nchi na pia hana tena uwezo wa kuongoza nchi.
No comments:
Post a Comment