Jeshila Marekani limewapiga marufuku wanajeshi wake nchini Japan kutokunywa pombe baada ya mwanajeshi mmoja kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani katika kisiwa cha Okinawa inayohusishwa na unywaji wa kupitia kiasi wa pombe.
Wanajeshi wa Marekani katika kisiwa hicho cha Okinawa pia wametakiwa kusalia katika kambi ama nyumbani.
Mwanajeshi huyo aliligonga gari lake na basi dogo siku ya Jumapili, na kumuua dereva wa basi hilo dogo.
Okinawa ina takriban nusu ya wanajeshi wote waliopo nchini Japan na wakaazi wamepinga kuwepo kwa wanajeshi hao.
Katika taarifa , jeshi la Marekani lilithibitisha kwamba mmoja wa wanajeshi wake alihusika na ajali hiyo na kuongezea kuwa pombe huenda ndio sababu.
Jeshi hilo pia lilitangaza mazoezi ya lazima ili kuangazia kuhusu utumizi wa pombe hatari kuwa na tabia njema miongoni mwa wanajeshi wake wote waliopo nchini Japan.
No comments:
Post a Comment