Tuesday, November 21

Utafiti: Uvimbe wa saratani ya matiti huwa ''mkubwa'' kwa wanawake wanene kupita kiasi

Mwanamke mneneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWanawake wenye unene wa mwili wa kupindukia wanahitaji kufanyiwa vipimo cha mara kwa mara cha kubaini saratani ya matiti vya mammograms
Ni vigumu kubaini chembe chembe za saratani ya matiti miongoni mwa wanawake wenye unene kupita kiasi kabla ya uvimbe kuwa mkubwa, umeeleza uchunguzi wa Sweden.
Wanawake wenye unene wa mwili wa kupindukia wanahitaji kufanyiwa vipimo cha mara kwa mara cha kubaini saratani ya matiti cha mammograms kusaidia kubaini uvimbe wa saratani, walisema watafiti, lakini wakaongeza kuwa ushahidi zaidi wa kubainisha hayo unahitajika.
Nchini Uingereza, wanawake wenye umri wa kati ya miaka 50 hadi 70 hualikwa kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya matitikila baada ya miaka mitatu.
Baadhi ya wanawake wenye hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti tayari hupata huduma ya uchunguzi wa mara kwa mara.
Hawa ni wanawake wanaotoka katika familia yenye historia ya saratani ya matiti , kwa mfano.
Kuwa na uzito wa mwili kupita kiasi pia huongeza hatari ya kupata saratani ya matiti, lakini kwa sasa si suala linalozingatiwa inapokuja katika muda wa kufanya vipimo vya saratani.
Taasisi ya Karolinksa iliwahusisha wanawake 2,012 waliopatikana na saratani ya matiti baina ya mwaka 2001 na 2008.
Uchunguzi wa saratani ya matitiHaki miliki ya pichaSPL
Image captionWanawake wenye hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti mfano wale wanaotoka katika familia zenye historia ya saratani hiyo wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara
Wanawake hao wamekuwa wakifanyika vipimo vya kutambua saratani ya matiti, vinavyofahamika kwa lugha ya kitaalam kama mammograms kila baada ya miezi 18 hadi miaka miwili kama tinavyoshauriwa shauriwa nchini Sweden.
Wanasayansi hao walichunguza juu ya ni vipi uvimbe mkubwa wa saratani wa kila mmoja wakati ulipobainika na pia uzito wa mwili wa mwanamke (BMI), kama kipimo cha uzito wa kupindukia.
Jopo hilo lilibaini kuwa wanawake waliokuwa na uzito wa kupita kiasi wa mwili walikuwa na uwezekano mkubwa wa pia wa kuwa na uvimbe mkubwa ulipobainika kwa kutumia njia ya mammogram ama wakati wa uchunguzi wa kawaida.
Hii ni kwasababu labda matiti yao yalikuwa makubwa na kwa hivyo ilikuwa ni vigumu kubaini uvimbe nama ni kwasababu uvimbe wao ulikua kwa kiwango cha haraka zaidi, aliieleza BBC mkuu wa utafiti huo Fredrik Strand.
Uvimbe mkubwa huwa unakuwa na chembe chembe mbaya za saratani, alisema.
Daktari Strand alisema : " Utafiti wetu unaonyesha kwamba pale daktari wa kliniki anapoonyesha athari na faida za kupima saratani ya matiti kwa mgonjwa mwenye uzito wa kupita kiasi wa mwili(BMI) lazima ieleweke kuwa ni muhimu.
" Zaidi ya hayo utafiti wetu unaonyesha kuwa wenye unene zaidi wa mwili wanapaswa kufanyiwa vipimo baada ya muda mfupi zaidi ."
Lakini Sophia Lowes, kutoka kituo cha utafiti wa saratani nchini Uingereza -Cancer Research UK, anasema kuwa utafiti ambao unawasilishwa kwenye mkutano wa mwaka wa taasisi ya Marekani ya utafiti wa matibabu ya saratani-Radiological Society of North America, haukutoaushahidi wa kutosha juu ya mabadiliko na ni kwa muda gani mwanamke anapaswa kufanyiwa uchunguzi.
Uchunguzi wa matiti unafaida na hasara zake, alisema Daktari Sophia Lowes, na kuongeza kuwa:"Husaidia kunusuru maisha kwa kubaini saratani ya matiti katika hatua zake za mwanzo,lakini kwa upande mwingine huwadhuru.''
Wanawake kwani baadhi ya wanawake hutambua saratani ambazo pengine zisingeweza kusababisha matatizo katika kipindi chao cha maisha.

No comments:

Post a Comment