Sunday, November 12

Mwanariadha aliyefungiwa hajui kama alitumia dawa za kusisimua misuli


Arusha. Shirikisho la Riadha nchini (RT) wiki iliyopita liliwafungia wanariadha Elia Sidame na Msenduki Ikoki bada ya kugundulika kutumia dawa aina moja ya Norandrostorene kwa nyakati tofauti katika mashindano waliyoshiriki mwaka jana na mwaka huu nchini China na Brazil walipokuwa kwenye mialiko yao binafsi.
Sidame alishiriki mashindano mawili nchini Brazil katika Jiji la Rio de Janeiro, Meia Maratona International Oktoba 16 na Circuito da Longividade Novemba 13 mwaka huo huo na kumaliza nafasi ya tano katika mashindano yote mawili na vipimo vya mashindano yote alipatikana na kosa la kutumia Norandrostorene.
Mwanariadha Msenduki yeye alishiriki mbio za CXD Xiamen International Marathon januari 2 mwaka huu na kumaliza nafasi ya nne huko Nchini China naye alikutwa na hatia ya kutumia dawa hizo hizo.
Hata hivyo, Sidame amesema kuwa hakutegemea kama angeweza kupata kifungo hicho kwa kuwa hajui ni kwa namna gani alitumia dawa hizo katika mbio za mialiko yake ambayo yalifanyika kwa wakati tofauti sio Tanzania tu.

No comments:

Post a Comment