Sunday, November 12

Wabunge 40 Uingereza hawana imani na May

Jumla ya wabunge 40 wa chama tawala nchini Uingereza cha Conservative wamekubaliana kusaini barua ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Theresa May.

Theresa May London (Reuters/T.Melville)
Taarifa hizo zimeripotiwa leo Jumapili (12.11.2017) na Gazeti la Sunday Times, na kwamba idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na ile ya wabunge 48 ambao wanahitajika kushinikiza kufanyika uchaguzi mpya, ambao huenda ukamuondoa May madarakani.
May amekuwa katika shinikizo kutoka ndani ya chama chake cha Conservative kutokana na uchaguzi mkuu wa mapema uliofanyika Juni 8, ambapo chama hicho bila kutarajia kilipoteza wingi wa kura bungeni. Utawala wa May pia umekosolewa jinsi unavyoyashughulikia mazungumzo ya Uingereza kujionda kwenye Umoja wa Ulaya, mchakato unaojulikana kama Brexit.
Wakosoaji wamesema kuwa awamu sita za mazungumzo ya Brexit kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya, yamepiga hatua kidogo sana na hayana uwazi wa kutosha kuhusu mchakato mzima wa kujiondoa kwenye umoja huo pamoja na ratiba kamili.
Barua ya siri kwa May yagundulika
Wakati huo huo, taarifa nyingine iliyochapishwa leo na gazeti la Jumapili la Mail, imegundua barua ya siri kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Boris Johnson na Waziri wa Mazingira, Michael Gove, inayomtaka May kushinikiza mipango migumu ya Brexit.
Boris Johnson Michael Gove London (Getty Images/C.J.Ratcliffe)
Boris Johnson na Michael Gove
''Ikiwa tunataka kukabiliana na wale wanaotaka kuuharibu mchakato huo, kuna njia za kusisitiza kuhusu namna ya kulitatua hilo,'' wamesema mawaziri hao. Mawaziri hao wamewambia May ''afafanue mawazo'' ya mawaziri walioko katika baraza lake la mawaziri ambao wanaunga mkono mipango myepesi katika mchakato wa Brexit na
Kwa mujibu wa gazeti la Mail, Johnson na Gove wametaka mipangilio ya kipindi cha mpito kwa ajili ya nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya ikamilike Juni 20, mwaka 2021.
Mawaziri hao wa mambo ya nje na mazingira, walipiga kampeni kuunga mkono Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya katika kura ya maoni ya 2016, huku May akiunga mkono kambi ya waliokuwa wanataka nchi hiyo ibakie kwenye umoja huo.
Aidha, akizungumza katika kipindi cha Andrew Marr kinachoroshwa na Shirika la Utangazaji la BBC, Waziri Gove amesema hatomzuia May iwapo ataamua kuongeza kiwango cha fedha anazotakiwa kilipa katika mchakato wa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya. Amesema hawezi Kumzuia May kufanya kile ambacho anakiona kuwa ni sahihi.
Amesema haamini kama ni muda muafaka wa kujiondoa katika mazungumzo ambayo yanasuasua kutokana na kiwango cha fedha ambacho Uingereza inapaswa kuchangia kabla ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya. Uingereza ambayo imekuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 1973, imekuwa ni nchi ya kwanza kuanzisha mchakato wa kujiondoa katika umoja huo.

No comments:

Post a Comment