Kutokana na adha hiyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pololet Mgema aliwaomba Watanzania, wafanyabiashara na wadau wenye nia njema kuchanga Sh19 bilioni zitakazotumika kujenga Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.
Mgema ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea alisema kukamilika kwa hospitali hiyo ya Namtumbo kutaokoa maisha ya watu ambao hufariki dunia wakiwa njiani kufuata huduma mkoani.
Alisema hospitali hiyo ikikamilika itawasaidia watu 200,000 wa Wilaya ya Namtumbo na za jirani.
Mgema alisema tayari pazia la uchangiaji limefunguliwa na kwa awamu ya kwanza kupitia mbio za Namtumbo wanatarajia kukusanya Sh1.2 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha upasuaji na wodi ya wazazi.
“Tukifanikisha kujenga wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji, tutapunguza vifo wakati wa kujifungua na itasaidia pia kuipunguzia mzigo hospitali ya mkoa.
“Huduma za upasuaji nazo ni muhimu, katika mkoa mzima hatuna hospitali kubwa ya wilaya inayotoa huduma hizo ingawa tumeanza kidogo kule Madaba na Manispaa ya Songea,” alisema Mgema.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Luckness Amlima alisema kutokana na umuhimu wa a hospitali hiyo amekuwa akitafuta njia mbalimbali kuhakikisha ujenzi wake unafanikiwa.
“Lengo la kujenga hii hospitali lipo muda mrefu nikaona nitafute namna tunayoweza kuwahamasisha watu wengine waweze kutusaidia ndipo wazo la marathon likaja,” alisema
No comments:
Post a Comment