Monday, November 27

Mugabe apewa sikukuu ya taifa Zimbabwe

Mugabe alikuwa ameongoza Zimbabwe tangu uhuru 1980Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMugabe alikuwa ameongoza Zimbabwe tangu uhuru 1980
Serikali ya Zimbabwe imetangaza siku kuu mpya ya kukumbuka mchango wa Robert Mugabe ambaye aliondolewa madarakani wiki iliyopita.
Gazeti la serikali la Herald limesema sikukuu hiyo itakuwa ikiadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa Bw Mugabe kila mwaka.
Uamuzi wa kusherehekea Siku ya Taifa ya Vijana ya Robert Gabriel Mugabe kila 21 Februari ulifanywa rasmi kupitia tangazo rasmi kwenye gazeti la serikali.
Tangazo hilo lilichapishwa Ijumaa - siku ambayo Rais Emmerson Mnangagwa aliapishwa kuwa rais, na kufikisha kikomo uongozi wa Mugabe wa miaka 37.
Serikali ya Bw Mugabe ilikuwa imeamua kutangaza siku ya kuzaliwa kwake kuwa sikukuu ya taifa mwezi Agosti, baada ya kampeni kutoka kwa mrengo wa vijana katika chama cha Zanu-PF.
Image captionRaia walimshangilia rais Mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa siku ya kuapishwa kwake
Bw Mugabe aliondolewa mamlakani wiki iliyopita kutokana na shinikizo kutoka kwa wanajeshi waliokuwa wamechukua udhibiti wa serikali wiki iliyotangulia.
Alijiuzulu na Bw Mnangagwa, makamu wa rais aliyekuwa amefutwa kazi wiki iliyotangulia na kutorokea nje ya nchi, akarejea na kuchukua usukani na kuapishwa Ijumaa baada ya Bw Mugabe kushurutishwa kujiuzulu.

No comments:

Post a Comment