Jeshi la anga la Marekani linaeleza kwamba limeanzisha mazowezi ya pamoja ya kijeshi kwa kutumia ndege mbili aina ya B-1B kutoka kambi ya jeshi ya Guam zikisindikizwa na ndege za kijeshi kutoka Korea Kusini na Japan Alhamisi kuelekea kwenye Peninsula ya Korea.
Shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini-KCNA Ijumaa limekosoa vikali mazowezi hayo na kuyaeleza ni mazowezi yanayotazamiwa kufanya shambulizi la kushtukiza la nyuklia.
KCNA limeeleza kwamba ukweli unadhihirisha wazi wahuni kama mabeberu wa Marekani wanaharibu zaidi hali katika peninsula ya Korea na kutaka kuanzisha vita vya nyuklia.
Mazowezi hayo yanaanza siku moja kabla ya kuanza ziara ya siku 12 ya rais Donald Trump huko Japan, Korea Kusini, China, Vietnam na Ufilipino, huku jeshi la anga limeeleza safari ya ndege hizo haikuanza kwa sababu ya tukio lolote lile kwa hivi sasa.
No comments:
Post a Comment