Friday, November 3

Trump alalamikia programu ya uhamiaji Marekani

DV Lottery Green Card
Shambulizi la ugaidi lililotokea Jumanne katika jiji la New York haraka limekuwa suala la kisiasa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kulalamikia program ya Diversity Visa Lottery Program - maarufu kama green-card.
Trump amesema kuwa program hiyo ndiyo iliyo mruhusu mshukiwa Sayfullo Saipov kuingia nchini Marekani.
Saipov ambaye aliwaambia maafisa kwamba aliamua kufanya shambulizi hilo siku ya haloween, kwa sababu alidhani watu wengi watakuwa mitaani. Alisomewa mashtaka jana Jumatano kwa makosa mawili ya uhalifu.
Rais Trump alisema anataka kufanya kazi haraka na bunge kufuta program hiyo ya visa kwa wahamiaji ambayo ilimruhusu Saipov kuingia Marekani.
Matamshi hayo yalipata ukosoaji kutoka kwa wademocrat ambao walisema kwamba Rais aliharakisha kuweka tukio hili la kisiasa wakati ambapo idara ya sharia inajaribu kuchunguza uhalisia wa kile kilichotokea.
Jana Jumatano Rais Trump katika ujumbe wa Twitter alimlaumu kiongozi wa baraza la seneti, mdemocrat Chuck Schumer wa New York kwa kuruhusu ugaidi ndani ya Marekani kama sehemu ya kile alichokiita uteteaji wake kwa mpango wa Diversity Visa Lottery Program.
Wakati huo huo Seneta Schumer alimshutumu Rais Trump kwa maneno yake kulifanya suala hili kisiasa na kuigawa Marekani, kitu ambacho anaonekana muda wote kukifanya pale linapotokea janga la kitaifa.
Seneta Schumer alisema muda wote anaamini na kuendelea kuamini kwamba uhamiaji ni jambo zuri kwa Marekani.

No comments:

Post a Comment