Akizungumza na waandishi leo Jumatano, Solomon amesema licha ya kuzuia mitihani hiyo uongozi wa chuo hicho umegushi matokeo ya mitihani ya wahitimu jambo ambalo ni makosa kisheria.
"Kutokana na mgogoro huu nimemwandikia Waziri wa Elimu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, TCU na Necta, kuelezea mgogoro huo wa kugushi matokeo ya wanafunzi wa Stashahada ya Ualimu na Uongozi ya Chuo Kikuu cha Mount Meru kutokana na ukiukwaji wa taratibu za kutolewa kwa matokeo chuoni hapo," amesema.
Akizungumzia hilo kaimu makamu mkuu wa chuo hicho, Utawala na Fedha, Twazihirwa Mzava amesema kuwa uongozi wa chuo hicho ulilazimika kuwapatia matokeo wanachuo hao nje ya taratibu baada ya mhadhiri kutokuwasilisha matokeo ya mitihani hiyo kwa uongozi wa chuo kutokana na kudai stahiki zake ambazo alikuwa hajalipwa.
Mzava amesema mhadhiri Solomon hakuwasilisha matokeo kwa sababu anadai stahiki zake kwa kipindi kirefu na hiyo inatokana na ukata unaokikabili chuo hicho.
No comments:
Post a Comment