Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inaongozwa na meya Alex Kimbe kutoka Chadema, huku CCM ikiwa na madiwani wanne kati ya 18 wa kuchaguliwa.
Akihutubia mkutano wa kumnadi mgombea wa CCM, Baraka Kimata, Mwamwindi alisema uongozi wa halmashauri hiyo umeshindwa kufanya kazi za kuwaletea maendeleo wananchi, badala yake umekuwa ukiendesha siasa za chuki na ubaguzi.
“Hali ilivyo ninyi wenyewe ni mashahidi, hakuna miradi ya maana ya maendeleo iliyoanzishwa na uongozi wa sasa, miradi yote ya barabara hata ujenzi wa stendi mpya ya mabasi ni ile tuliyoipanga sisi,” alisema Mwamwindi.
Naye diwani wa Mshindo, Ibrahim Ngwada alisema CCM inahitaji kuongeza nguvu ya diwani huyo ili washiriki kupambana na vitendo vinavyofanywa kwenye baraza la madiwani ambavyo havina masilahi kwa umma.
Alisema tangu baraza hilo lianze kazi limepitisha mambo kadhaa ambayo hayana masilahi kwa umma, badala yake ni kuleta hasara.
Kimata, ambaye alikuwa diwani wa kata hiyo kupitia Chadema aliyejiuzulu miezi miwili iliyopita, aliwataka wakazi wa kata hiyo kumchagua ili aweze kuwaletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment