Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 11, Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi ,Mkoa wa Singida,Isaya Mbughi, amesema ajali ambayo imetokea Ikungi mkoani humo imesababisha vifo vya watu wawili.
Kamanda Mbughi amesema miili ya abiria hao wa ambao majina yao wala makazi yao bado hayajulikana, imehifadhiwa katika hospitali ya misioni Puma.
Kamanda Mbughi amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa kuna kila dalili dereva wa gari ndogo alikuwa amelala na gari lilihama kutoka upande wa kushoto,na kwenda kulia.
“Dereva wa basi amejitahidi mno kukwepa gari hilo ndogo,lakini ilishindikana na hivyo kuingia uvunguni mwa basi.Kwa wakati huo,basi lilihama upande wake wa kulia na kwenda nje ya barabara,lakini alilifuata huko huko”,amesema
Wilayani Hai ,mkoani Kilimanjaro watu watano wamepoteza maisha na wengine wanne wakijeruhiwa baada ya lori kugongana uso kwa uso na Noah maeneo ya kikavu kwa Sadala.
Daktari wa zamu hospital ya wilaya ya Hai,Agness Temba amesema amepokea miili ya watu wa tano.
Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Hai, na majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi.
No comments:
Post a Comment