BoT kupitia Idara ya Uhusiano na Itifaki ilitoa taarifa kwa umma jana Ijumaa Novemba 3,2017 kutokana na kuwepo taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kushuka kwa thamani ya Shilingi.
“BoT inapenda kuufahamisha umma kuwa kuna hazina ya kutosha ya fedha za kigeni na hakuna sababu ya taharuki,” imesema taarifa hiyo.
Benki Kuu imesema hadi kufungwa kwa soko la jumla la fedha za kigeni linaloendeshwa na BoT jana Ijumaa jioni Novemba 3,2017, Shilingi ya Tanzania ilikuwa inauzwa kati ya Sh2,246.50 na Sh2,247.60 kwa Dola ya Marekani.
“Hata hivyo, saa 12:30 jioni ya Novemba 3,2017 takwimu za Bloomberg zilionyesha thamani ya Shilingi kushuka hadi kufikia Sh2,481.83 kwa Dola ya Marekani -taarifa ambayo si sahihi,” imesema taarifa ya BoT.
Benki Kuu imesema baada ya mawasiliano na Bloomberg (kampuni inayohusika na masuala ya data za kifedha, biashara na masoko) ilionekana kuna baadhi ya wachangiaji waliingiza takwimu zisizo sahihi na hivyo marekebisho yakaanza kufanyika.
No comments:
Post a Comment