Saturday, November 4

Tazara yahitaji Sh2.7,trilioni kuboresha,miundombinu


Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) imesema inahitaji Dola 1.2 bilioni za Marekani (sawa na Sh2.7 trilioni), kuboresha miundombinu yake ili watoe huduma kwa ufanisi.
Wakati Tazara ikieleza hayo, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeishauri mamlaka hiyo kuandaa utaratibu wa safari za kutembelea utalii wa ndani kwa Watanzania kwa lengo la kukuza sekta hiyo muhimu kwa mustakabali wa uchumi wa nchi.
Hayo yalibainika jana katika hafla ya kufurahia urithi wa reli ya Tanzara kutangaza utalii wa ndani iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watanzania waliosoma China (CAAT).
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Tazara, Mhandisi Betram Kiswaga alisema tangu mamlaka hiyo ianzishwe miaka ya 1970 haijawahi kufanyiwa ukarabati mkubwa.
Awali, akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuliwa na Balozi wa China nchini, Wang Ke, Mwenyekiti wa TTB, Jaji mstaafu Thomasi Mihayo alitoa rai kwa menejimenti ya Tazara kuangalia jinsi ya kuutangaza utalii wa ndani ili kukuza uchumi wa Taifa.
“Tazara mnapaswa kuandaa safari za kila mwisho wa mwezi za kutembelea vivutio vya ndani, inaweza kusaidia kukuza utalii wetu na kama mlivyosikia Balozi wa China alivyosema, tutashirikiana nao hivyo hii ndiyo fursa tuitumie,” alisema Jaji Mihayo.
Kuhusu ombi hilo, Mhandisi Kiswaga alisema hawana tatizo kwa kuwa huduma kama hiyo ilikuwapo awali, lakini kutokana na kudorora kwa huduma za Tazara walisitisha.

No comments:

Post a Comment