Kukwama kwa nyumba hiyo imefikisha idadi ya nyumba mbili kati ya tatu zilizokwama katika mnada ulioendeshwa na Kampuni ya Udalali ya Yono.
Nyumba hizo zinauzwa kwa amri ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufidia kodi anayodaiwa Lugumi Sh14 bilioni.
Mkurugenzi wa Yono, Scholastika Kevela amesema bei ya mwisho imefikia Sh650 milioni ambayo iko chini ya bei elekezi iliyopendekezwa na Serikali.
Katika mnada uliomalizika leo asubuhi Novemba 24 Mbweni JKT, nyumba ya Lugumi ilikosa mteja kwani walishindwa kufikia bei elekezi.
Mmoja wa wateja waliojitokeza Upanga Idd Kibula amesema "Mimi nilifikia Sh650 milioni lakini nimeambiwa iko chini hivyo hakuna jinsi. Tutaangalia tena ukitangazwa kama nitakuja.

No comments:
Post a Comment