Progrtamu hiyo itasaidia kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini.
Kwa mujibu wa kampuni hiyo, programu hiyo inahusisha uwekezaji mkubwa unaolenga kuhakikisha uhakika wa upatikanaji wa huduma ya 3G, ujazo wa data kamili pamoja na kuongeza kasi ya intaneti.
Akiongea wakati wa kutangaza huduma hiyo jijini Dar es Salaamn leo Novemba 9, Meneja Ubora wa huduma za Mtandao Airtel, Emanuel Luanda, amesema Airtel imedhamiria kuimarisha huduma ya mtandao kutokana na ongezeko la matumizi ya simu za smartphone kulikosababsiah kukua kwa mahitaji ya huduma hiyo.
“Kutokana na uboreshaji wa mtandao wetu, wateja wote nchini watakuwa wakitapa huduma yenye kasi na hivyo kuwa na uhakika na huduma bora kutoka Airtel wakiwa popote,” amesema.
Kwa mijibu wa Luanda ripoti ya hivi karibuni ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inayotoa mchanganuo wa matumizi ya huduma za Intaneti inaweka wazi kuweko kwa ongezeko la watumiaji wa huduma za intaneti kutoka asilimia 34 ya watanzania mwaka 2015 hadi aslimia 40 mwaka 2016.
“Hali hiyo ndio inatoa msukumo hata kwetu Airtel kuendelea kuwekeza zaidi katika teknolojia mpya ili kuwapatia wateja wetu huduma bora zaidi,” ameongeza.
Kwa upande wake, Meneja wa Masoko Airtel Tanzania, Arnold Madale amesema: “Kwa kuwa Airtel tunatambua mahitaji ya wateja wetu na hali ya soko, tumekuwa tukifanikiwa kuleta bidhaa zenye ubunifu na mpangilio wa huduma zinazozingatia mahitaji ya mteja.”
, hii ni hatua kubwa sana hasa kwenye ushindani wa biashara. Tunao wateja ambao wanatumia mtandao wetu kwa ajili ya intaneti tu, lakini pia kuna wale wanaotumia kwa kupiga na kupokea simu, tunazo bidhaa na huduma ambazo zinakidhi matakwa ya wateja hao kwa muda wote wakiwa mahali popote. Kwa sasa hivi tunaendelea pia kuboresha huduma yetu ya 2G ili kutoa huduma yenye uhakika wa hali ya juu ikiwemo huduma ya Airtel Money ili kuendelea kuwafikia Watanzania wengi waishio pembezoni huduma za kibenki na huku tukitimiza sera ya serikali ya kushiriki katika uboreshaji wa huduma bora za kifedha vijijini.”
“Tunapotangaza huduma hii muhimu ya kuboresha mtandao wetu, tunayo furaha kutangazia huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambayo inapatika kwa urahisi na kumfanya mteja kuwa na Uhuru zaidi wa kutumia Intaneti yenye kasi kwa muda mrefu zaidi kwa kuwasiliana na ndugu, marafiki au wadau katika biashara mahali popote. Wateja wetu wataweza kufaidi huduma hii ya bando kwa kupiga *150*60# na kujipatia 1GB, dakika150 kupiga mitandao yote na kudumu nazo kwa muda wa siku saba, aliongeza Madale.
‘Nia yetu ni kuendelea kukua kupita Maelezo huku tukitengeneza ujuzi wa kuaminiwa na wateja wetu kwa kuwa na gharama nafuu. Mradi wa U900 unadhihirisha kuwa Airtel imeamua kuinua taifa letu kufikia lengo la kuishi kidigitali kwa kuwepo na huduma za kidigitali, aliongeza Madale.
No comments:
Post a Comment