Balozi Amina amesema hayo leo Jumatatu katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea Zanzibar wakati akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Kikwajuni, Nassor Salum Ali.
Mwakilishi huyo alitaka kujua kuna sababu gani za msingi kwa Serikali kupiga marufuku uokotaji wa karafuu za mpeta wakati zilikuwa zinawaingizia fedha watu hasa wanawake.
Akijibu swali hilo Balozi Amina amesema kutokana na malalamiko mengi ya wanajamii kwa kuibuka matendo ya ubakaji kwa wanawake wanaokota karafuu za mpeta ndio maana kwa makusudi Serikali imeamua kupiga marufuku uokotaji wa aina hiyo.
“Utakuta wanawake wanatoka nyumbani kwao wakielekea Mkoani kuokota karafuu za mpeta huku wakiwa wamejipamba, hali ambayo huwa ni kishawishi kikubwa kwa wanaume kuwafanyia vitendo viovu vikiwamo vya ubakaji, hivyo upigaji marufuku huu tunaamini utasaidia sana kurudisha heshima za wanawake,” amesema.
Amesema kutokana na agizo hilo Serikali imeandaa adhabu kali kwa yule atakayepigana na agizo hilo kwa kuchukuliwa hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment