Akizungumza katika uzinduzi huo leo Jumatatu Mkuu wa Sheria na Uhusiano wa Total Tanzania, Marsha Msuya amesema katika kufanikisha mpango huo, wameshirikiana na shirika la Safe Communities linalofanya shughuli za elimu na utafiti wa usalama barabarani.
Amesema mpango huo wa elimu ya usalama barabarani umeanza leo Jumatatu na utaendelea kwa muda wa wiki moja na utafanyika utafiti wa kuangalia mwenendo wa wanafunzi baada ya kupatiwa elimu hiyo.
"Elimu hii itafanyika katika shule 10 za wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam zikiwemo shule za msingi Veternary na Mbagala za wilaya ya Temeke, Vijibweni na Kibada za Kigamboni, Kinondoni na Magomeni Lions za Kinondoni, Mpakani na Ukombozi za Ubungo pamoja na Juhudi na Mwangaza za Wilaya ya Ilala," amesema Marsha.
Amesema kampeni hiyo ni matokeo ya mkakati mkubwa ujulikanao kama 'On the Road to safety A DECADE FOR ACTION" uliozinduliwa rasmi na kampuni ya Total mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment