Tuesday, October 3

Wanaharakati wakataa msaada wa mke wa Mugabe



Mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe
Mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe 
Harare, Zimbabwe. Mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe ameshutumiwa na wataalamu wa afya na wanaharakati baada ya kudaiwa kutoa msaada wa nguo za ndani zilizotumika kwa wanachama wa Zanu-PF mjini Mutare.
Kwa mujibu wa gazeti la NewsDay, msaada huo ulikabidhiwa kwa wafuasi hao na mfanyabiashara mashuhuri na Mbunge wa Chikanga –Dangamvura, Esau Mupfumi aliyedai umetolewa na mke wa rais.
"Hivi karibuni nilikwenda Ikulu ambako nilikutana na Grace Mugabe na alinikabidhi nguo hizi ili niwapatieni. Ninazo hapa na nimeambiwa zenu haziko katika hali nzuri kwa hiyo tafadhali njooni mchukue leo. Kuna nguo za kulalia, ndala na nguo, njoni mchukue, hizi zinatoka kwa Grace Mugabe," gazeti lilimnukuu Mupfumi akisema.
Kadhalika ripoti ilimnukuu mnufaika mmoja wa chupi hizo ambaye hakutaka jina lake litajwe akimlaumu Grace kwa kuwapatia kama msaada badala ya kutengeneza ajira ili kumaliza tatizo la ukosefu wa kazi katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
"Haya ndiyo masuala yanayohitaji kuzungumziwa badala ya kutupatia nguo ya ndani. Hatuna kazi na kwa nini ametufanyia hivi?" alihoji mwanaharakati wa Zanu-PF.
Ripoti zilizotolewa na shirika la kazi la Zimbabwe Congress of Trade Unions ukosefu wa kazi nchini ni zaidi ya asilimia 85, ingawa shirika la takwimu la serikali linasema ukosefu wa kazi ni asilimia 11 tu.

No comments:

Post a Comment