Tuesday, October 24

UTALII WA NDANI WACHOMOZA NCHINI

PAMOJA na idadi kubwa ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini bado mchango wa sekta hiyo si wa kuridhisha kiasi cha kuasidia kupunguza bajeti ya Taifa.
Kwa mujibu wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka wa fedha 2017/2018 Sekta ya utalii imeendelea kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi nchini kwa sekta mbalimbali ikiwamo sekta za kilimo, mawasiliano, miundombinu, usafirishaji, burudani na uzalishaji wa bidhaa kwa watalii.
Katika mwaka 2016/2017 sekta ilichangia asilimia 17.5 ya pato la taifa huku ikilipatia taifa asilimia 25 ya fedha zote za kigeni.
Katika kipindi hicho pia zaidi ya watu laki tano waliajiriwa katika sekta ya utalii na wengine zaidi ya milioni moja walijiajiri wenyewe katika sekta hiyo.
“Sekta hii inachangia katika kuzalisha ajira na mapato ya serikali, uhifadhi wa mazingira na kutunza mifumo ikolojia kwa manufaa ya binadamu na wengine” inaeleza taarifa ya bajeti.
Mwaka 2016 mapato yanayokana na utalii yaliongezeka kufikia Dola za Marekani bilioni 2 ikilinganishwa na Dola za Marekani bilioni 1.9 zilizopatikana mwaka 2015.
Ongezeko la mapato hayo linaelezwa kutokana na kuongezeka kwa watalii wa nje 1,137,182 mwaka 2015 hadi watalii 1,284,279 mwaka 2016.
Aidha serikali ilifanikiwa kukusanya zaidi ya Sh bilioni 5.6 za maduhuli yanayotokana na ada za leseni za biashara za utalii ikilinganishwa na Sh bilioni 4.1 mwaka 2015 likiwa ni ongezeko la asilimia 36.
Ongezeko linaloelezwa kusababishwa na matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa usajili na utoaji leseni na ongezeko la kampuni zinazotoa huduma ya utalii ambapo ziliongezeka kutoka 1,087 mwaka 2015 hadi 1,244 mwaka 2016.
Pamoja na umuhimu wa sekta hii ambayo hata hivyo haijaweza kufikia kiwango cha uchangiaji katika pato la Taifa ikilinganishwa na ukubwa wake kwa kuwa na idadi kubwa ya vivutio vya utalii na vy kipekee.
Utalii wa ndani ambao ni muhimu kwa ustawi wa sekta nzima bado haujaweza kuwa wenye tija kutokana na idadi ndogo ya watalii wa ndani inayosababishwa na mwamko mdogo wa wananchi na kukosekana kwa ushawishi wa kuwavutia na kuwafanya waone wanao wajibu wa kushiriki katika shughuli za utalii ndani ya nnchi yao.
Kutokana na hali hii Serikali ina mpango gani kuhakikisha inaongeza mapato ya utalii kwa kuoingeza idadi ya watalii hasa watalii wa ndani.
Devota Mdachi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) anasema tangua mwezi Agosti mwaka huu wameanza kutekeleza kampeni maalumu ya kukuza utalii wa ndani inayofahamika kama Utalii wa Mtanzania utaanza na Mtanzania mwenyewe.
Anasema kampeni hii inayorushwa kupitia vipindi mbalimbali vya redio kama vile Redio Free Afrika, Magic FM, Clouds, East Afrika Redio na Tbc.
Baadhi ya televisheni zinazotumika kurusha kurusha kampeni hivyo ni pamoja na TBC, ITV, Star TV, Clouds, ATN na Channel Ten.
“Bodi imeshirikiana na “wanablogs” mbalimbali nchini katika kutangaza utalii kupitia mitandao ya kijamii” anasema.
Devote anasema anasema kupitia kampeni hiyo ya itakayodumu kwa miezi sita hadi mwanzoni mwa mwezi uliopita iliwasaidia kuongeza watu wanaofualia mitandao yao ya kijamii tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
Anasema katika kipindi hicho watu walifuata mtandao wao wa twitter waliweza kuongezeka hadi kufikia 905, wafuatiliaji wa Instagram  waliongezeka kufikia zaidi ya 12,000 huku wale wa facebook wakifikia 76,000.
Utangazaji wa kutumia mabango katika miji mbalimbali hususani katika miji mikubwa ili kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu utalii wa ndani.
Jumla ya mabasi 300 yamewepewa filamu maalumu za kushawishi utalii kwa kuonesha vivutio hivyo mpango utaowalenga zaidi watu wanaotumia usafiri huo kuelekea mikoa mbalimbali nchini.
Kwa mujibu wa Devota baada ya kuwekwa kwa filamu hizo wamekuwa wakipokea simu nyingi zinazoulizia kuhusu masuala mbalimbali ya utalii.
Anasema wako katika mkakati wa kuanza mpango wa kukuza utalii wa ndani kwa makundi maalumu kama vile wafanyakazi, wanafinzi na waumini wa dini mbalimbali kupitia vikundi vyao vya sehemu za ibada.

No comments:

Post a Comment