Njwete anayewakilishwa na wakili Juma Nassoro anadaiwa kutenda makosa hayo Septemba 6,2016 saa nne usiku eneo la Buguruni wilayani Ilala, Dar es Salaam.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumanne Oktoba 31,2017 baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi ukiwa na mashahidi 10.
Hakimu Mkazi, Flora Haule akitoa uamuzi amesema Mahakama imemuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu baada ya kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani.
Mshtakiwa amesema atajitetea kwa njia ya kiapo na ana mashahidi wawili.
Kesi imeahirishwa hadi Novemba 14,2017 kwa ajili ya mshtakiwa kuanza kujitetea.
No comments:
Post a Comment