Tuesday, October 3

Rais Uhuru amtuma Ruto kumwakilisha kwenye Tume ya Uchaguzi


Rais Uhuru Kenyatta amemtuma Makamu wa Rais William Ruto kuhudhuria kikao kilichoitishwa naTume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) licha ya maelekezo yaliyotaka wagombea urais kufika wenyewe.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema wagombea urais watapaswa kuhudhuria wao wenyewe badala ya kuwatuma wawakilishi wao.
Ruto amewasili kwenye jengo la Bomas of Kenya, Nairobi saa 10:15 alasiri akiwa pamoja nakiongozi wa wabunge wengi Seneta Kipchumba Murkomen (Elgeyo Marakwet) na Aden Duale (Garissa Mjini).
Waliwasili muda mfupi baada ya viongozi wa muungano wa upinzani wa Nasa wakiongozwa na Raila Odinga kumaliza kikao chao. Raila aliongozana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, seneta wa Bungoma Moses Wetang'ula (Ford Kenya), Musalia Mudavadi (ANC) na wa Siaya, James Orengo.
Orengo amewaambia waandishi wa habari kwamba kikao hicho hakikuwa na matunda yoyote akasema kitakuwepo kikao kingine siku zijazo.
Orengo alisema IEBC imewapa maelezo ya nini wanachofanya na siyo wanachotarajia kufanya ili kurekebisha makossa yaliyojitokeza katika uchaguzi wa Agosti 8 uliosababisha matokeo ya urais kufutwa.
"Lazima ufanyike ukaguzi kuhakikisha usalama na kuaminika kwa teknlojia itakayotumika. There should be an audit to ensure security and integrity of the technology to be deployed. IEBC haiku wazi katika hili," alisema.
Mazungumzo kama haya yalivurugika Jumatano iliyopita baada ya wawakilishi wa Nasa kutoka nje wakidai Jubilee hawakuwa na nia njema. Orengo alisema hiyo ilitokana na mapendekezo ya marekebisho ya sheria.

No comments:

Post a Comment