Polisi nchini Tanzania inaendesha msako mkali kumnasa muuzaji wa pombe ya kienyeji ''GONGO'' iliyo sababisha vifo vya watu nane
Waathirika wengine wamelazwa katika hospitali mjini wa Dar es Salaam baada ya kunywa pombe haramu.
Kwa mujibu wa Jeshi la polisi nchini humo miili ya marehemu hao ambao wana umri kati ya miaka 25 na 70 pamoja na sampuli ya pombe hiyo iliyopatikana katika eneo la tukio itapelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini aina ya kemikali iliyosababisha vifo hivyo.
Baraza la mji huo linaamini kuwa pombe hiyo ilikuwa na kemikali kwa jina GV , yenye rangi inayotumika kutibu maambukizi ya ugonjwa wa ngozi ambayo inatuhumiwa kusababisha vifo hivyo.
Huku pombe ya kienyeji ikitengezwa kutokana na mbegu ama hata mboga nyumbani, pombe nyengine zinadaiwa kutengezwa kwa kutumia kemikali hatari kwa lengo la kuvifanya vinywaji hivyo kulevya zaidi na hivyobasi kuvutia wateja zaidi.
Hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kufikia sasa kuhusiana na kisa hicho.
Kinywaji hicho cha kienyeji , hutumiwa zaidi ya vinywaji vingine kwa sababu ni bei rahisi ilikinganishwa na vinywaji vya kawaida.
Mamlaka katika mji huo imeshindwa kuzuia vinywaji haramu.
Maafisa wengine wa baraza la mji huo wanaaminika kuwa wateja ama hata hushiriki katika biashara hiyo.
No comments:
Post a Comment