Tuesday, October 10

Nyumba ya mchezaji aliyeshindwa kufunga mabao yavamiwa na mashabiki Zambia

Alex Ng'onga -wa tano kutoka kushotoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionAlex Ng'onga -wa tano kutoka kushoto
Polisi nchini Zambia wamewakamata mashabiki watano kwa madai kuwa walivamia nyumba ya mwanasoka wa timu ya taifa ya kandanda Alex N'gonga.
Mashabiki hao walishikwa na hasira kuwa Ng'onga. alikosa nafasi wazi za kufunga wakati wa mechi muhimu ya kufuzu kwa kombe la dunia ambapo Nigeria iliishinda Zambia bao 1-0
Mashabiki walitoa hasira zao kwa kuvamia nyumba yake iliyo mji wa Kitwe ambao waliitupia mawe, kwa mujibu wa kamishina wa polisi Charity Katanga.
"Tumekamata watu watano kwa makosa ya kuharibu mali na sasa wanazuiliwa ns polisi."
Kushindwa kwa Zambia kuliipokonya fursa ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Urusi ambapo Nigeria walifuzu.

No comments:

Post a Comment