Tuesday, October 31

Nape Nnauye afunguka kuhusu hili

 Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Nape Nnauye amefunguka na kuweka sawa kuwa siku ya kesho Oktoba 31, 2017 hatakuwa na mkutano wowote na vyombo vya habari na kusema kuwa watu wanatunga hizo taarifa.

Nape Nnauye ametoa kauli hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii na kuwataka watu waache kumzushia mambo wakiwa na lengo la kutafuta nafasi na vyeo serikalini.

"Acheni kupiga ramli juu ya kesho yangu!! Kisa mnatafuta vyeo na hamuwezi kutumia akili kufikiri! Sina 'press conference' kesho" aliandika Nape Nnauye

Leo mchana watu wasio na nia nzuri na Nape Nnauye walizusha taarifa kuwa kiongozi huyo siku ya kesho Jumanne atakuwa na mkutano na waandishi wa habari jambo ambalo yeye mwenyewe amelipinga na kusema watu wanazusha taarifa hizo kwa maslahi yao wenyewe.

No comments:

Post a Comment