Tuesday, October 31

Mwanasiasa wa upinzani ahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela Cameroon

Mwanasiasa wa upinzani ahukumiwa miaka 25 jela Cameroon
Image captionMwanasiasa wa upinzani ahukumiwa miaka 25 jela Cameroon
Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limeikosoa mahakama ya kijeshi nchini Cameroon kwa kumhukumu kiongozi mmoja wa upinzani miaka 25 jela kwa makosa ya kuchochea uasi.
Aboubakar Siddiki - kiongozi wa chama cha upinzani kaskazini mwa nchi, ndiye mwanasiasa aliyepelekwa jela katika harakati za Cameroon za kuuzima upinzani hivi karibuni.
Hakuna ushahidi uliotolewa mahakamani kuchangia hukumu kama hiyo , taarifa ya Amnesty International ilisema.
Alikamatwa mwaka 2014 baada ya kulaumiwa kwa kupanga kuipindua serikali ya Rais Paul Biya.
Bwana Biya amekuwa madarakani tangu mwaka 1982 na wakosoaji wake wanamtaja kuwa dikteta.
Watu kadhaa wameuawa na mamia kukamatwa wakati wa maandamano katika eneo hilo lenye watu wanaozungumza lugha ya Kiingereza na ambao wanalalamika kutengwa.

No comments:

Post a Comment