Wakazi wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuacha kufikiria kurudishiwa fedha wanazochangia kwenye Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kwa ajili ya matibabu wasipougua muda mrefu badala yake wamshukuru Mungu kwa kuwaepushia magonjwa.
Akizindua mpango wa bima ya afya kwa watoto maarufu ‘Toto Afya Kadi’, Mkuu wa mkoa huo, Aggrey Mwanri alisema kuugua si jambo zuri.
“Tunapaswa kumshukuru Mungu pale tunapoishi bila kuugua na kuachana na kuwazia kurudishiwa fedha tulizochangia, maana fedha hizo huwezi kuzilinganisha na usalama wa afya yako,” alisema Mwanri.
Naye Meneja wa NHIF Mkoa wa Tabora, Vedastus Kalungwana alisema mpango huo utawapa fursa watoto chini ya miaka 18 kutibiwa wakiwamo wanafunzi. Alisema miongoni mwa watakaotibiwa ni watoto walio katika mazingira magumu wakiwamo yatima.
No comments:
Post a Comment