Nicol ambayo ilianzishwa Juni 25, 2003 na watu wachache kabla ya kuuza hisa zake kwa umma Machi 6, 2004 ili kukuza mtaji wake.
Hata hivyo, kwa kipindi cha miaka 13 ilikuwa haijatoa gawio hadi juzi ilipotangaza kuwa Sh946 milioni zimetengwa kwa ajili hiyo baada ya kampuni hiyo kupata faida ya Sh8.67 bilioni baada ya kodi.
Kutokana na shughuli zake za msingi, kampuni hiyo iliyoanzishwa ikiwa na mtaji wa Sh140 milioni kutoka kwa wanahisa 148, mapato yake yalikuwa Sh1.912 bilioni ambayo ni takriban mara tatu ya vyanzo vyake vingine ambako iliingiza Sh6.1 bilioni.
Ingawa mapato ya msingi mwaka 2016 yalipungua yakilinganishwa na Sh2.02 bilioni ilizoingiza mwaka 2015 na kupata faida ya Sh15 milioni, Nicol ilifanya marekebisho muhimu ya kupunguza gharama za uendeshaji.
Marekebisho hayo yamefanikiwa kupunguza gharama za mikopo kwa zaidi ya Sh1.5 bilioni kutoka Sh1.618 bilioni mwaka jana mpaka Sh42.037 milioni huku zile za utawala zikishuka kutoka Sh2.691 bilioni mpaka Sh2.667 bilioni ndani ya muda huo.
Juhudi za kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Nicol, Dk Gideon Kaunda aliyesaini taarifa hizo hazikuzaa matunda kwani alipotafutwa kwa simu ya ofisini msaidizi wake alisema ana jambo analishughulikia hivyo atafutwe baadaye. Hata ilipopigwa baada ya muda uliopendekezwa ili kupata ufafanuzi wa kampuni hiyo kutumia zaidi ya Sh2.6 bilioni kugharamia shughuli za utawala ilhali mapato yake yakiwa Sh1.9 bilioni, ilielezwa kuwa yupo nje ya ofisi.
Lakini kumbukumbu zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ilifutiwa usajili kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) mwaka 2011 baada ya kushindwa kuchapisha taarifa za fedha kwa miaka miwili mfululizo, mwaka 2009 na 2010. Licha ya hilo, Nicol ilibainika kufanya baadhi ya maamuzi bila kuushirikisha uongozi wa soko hilo kama inavyoagizwa kisheria kwa kampuni zote zilizokamilisha vigezo kwa kushiriki DSE.
Kampuni hiyo inamiliki hisa kwenye taasisi nane zenye thamani ya zaidi ya Sh97.728 bilioni pamoja na amana za Benki Kuu (BoT) za Sh30 milioni tangu mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment