Tuesday, October 17

Marekani yataka utulivu baada ya wanajeshi wa Iraq kuingia Kirkuk

Iraqi forces flash a victory sign while driving past an oil production plant near Kirkuk. Photo: 16 October 2017Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionWanajeshi wa Iraq wakisherehekea ushindi
Marekani imeomba kuwepo utulivu baada ya wanajeshi wa serikali ya Iraq kuingia mji wa Kirkuk kaskazini mwa nchi hiyo na kutwaa udhibiti wa maeneo muhimu kutoka kwa Wakurdi.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Heather Nauert amezitaka pande zote kuzuia makabiliano zaidi.
Wanajeshi wa Iraq walielekea Kirkuk wiki tatu zilizopita, baada ya jimbo la Kurdistan kuandaa kura ya maoni ya uhuru iliyokumbwa na utata.
Lengo lao limekuwa ni kuteka sehemu zilizo chini ya udhibiti wa Wakurdi waliochukua usukani baada ya Islamic State kuondoka eneo hilo.
Wenyeji wa maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Wakurdi ukiwemo mji wa Kirkuk, kwa wingi waliunga mkono kujitenga kutoka kwa Iraq wakati wa kura ya tarehe 25 mwezi Septemba.
Map showing Iraqi Kurdistan and areas controlled by Kurdish forces
Image captionRamani ya maeneo yanayodhibitiwa na vikosi vya kurdi
Licha ya mji wa Kirkuk kuwa nje ya eneo la Kursistan, wapigaji kura wa Kurdistan walio mjini humo waliruhusiwa kushiriki kura hiyo ya uhuru.
Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi aliitupilia mbali kura hiyo na kuitaja kuwa iliyo kinyume na katiba.
Huku hayo yakijiri, wapiganaji wanaoungwa mkono na serikali wamechukua udhibiti wa mji wa Sinjaar Kaskazini magharibi mwa mkoa wa Nineveh.
Hatua hiyo katika mji unaodaiwa na wakurdi na pia mamlaka za Iraq, ilifanyika bila ya kuwepo mapigano baada ya wanajeshi wa Wakurdi wa Peshmerga kuondoka eneo hilo.
Iraqi forces near an oil facility in Kirkuk, Iraq (16 October 2017)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJeshi la Iraq limedhibiti vituo vya mafuta
Katika taarifa Bi Nauert alisema kuwa Marekani ina wasiwasi kutokana na ripoti za kuendelea mapigano katika mji wa Kirkuk.
Bi Nauert alisema kuwa Marekani ilikuwa ikishirikiana na maafisa kutoka pande zote, kushiriki mazungumzo ikionya kuwa bado kuna kazi kubwa ya kulishinda kundi la Islamic State nchini Iraq.
Mapema Rais Donald Trump alikuwa amesema kuwa maafisa wa Marekani hawapendelei upande wowote.

No comments:

Post a Comment