Tuesday, October 17

Mahakama yaondoa marufuku ya maandamano Kenya

Mahakama yaondoa marufuku ya maandamano KenyaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMahakama yaondoa marufuku ya maandamano Kenya
Mahakama kuu nchini kenya imeondoa kwa muda marufuku kwa maandamano dhidi ya tume ya uchaguzi ya chi hiyo IEBC.
Muungano wa upinzani (Nasa) ulikuwa tayari umetangaza kuwa haungefanya maandamano leo dhidi ya tume ya uchaguzi, ili kuwaruhusu viongozi wake kuwatembelea watu walipigwa na polisi wakati wa maandamano.
Katika taarifa, msemaji wa kiongozi wa Nasa, Raila Odinga, Dennis Onyango, alisema kuwa watasitisha maandamano leo kuonyesha huruma kwa wale waliojeruhiwa na polisi wakati wa maandamano.
Nasa imewalaumu polisi kwa kutumia nguvu nyingi dhidi ya waandamanaji, madai ambao polisi wamekana.
Mwanafunzi aliuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumatatu wakati wa maandamano mjini Kisumu, magharibi mwa Kenya.
Maandamano yalizuka baada ya uchaguzi wa mwezi Agosti, ulioshindwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Mahakama ya juu zaidi iliamua kuwa uchaguzi huo ulikuwa na hitilafu.
Bw. Odinga anasema hatashiriki marudio ya uchaguzi wa wiki ijayo kwa sababu matakwa yake kwa tume ya uchaguzi kufanyiwa mabadiliko hayajatekelezwa.

No comments:

Post a Comment