Saturday, October 14

Mama wa mgombea urais wa Rwanda adai kuteswa

Adeline Rwigara
Mama wa aliyekuwa mgombea urais wa Rwanda ameiambia mahakama mmoja nchini Rwanda kuwa aliteswa akiwa rumande, shirika la Associate Press limeripoti Ijumaa.
Adeline Rwigara pia amesema Ijumaa kuwa alinyimwa chakula na maji kwa muda wa siku tano.
Lakini kwa mujibu wa vyanzo vya habari Jaji alimnyamazisha asiongee wakati kesi inasikilizwa Mahakama ya Nyarugenge.
Mwanamke huyo ni mama wa Diane Rwigara, mwanaharakati wa haki za binadamu ambaye amesema kuwa tuhuma zilizofunguliwa dhidi ya familia yake ni uzushi na kuwa zinatokana na kuikosoa serikali kwa rikodi yake ya uvunjifu wa haki za binadamu.
Rwigara, mama yake na dada yake Anne wamekanusha tuhuma za uchochezi na "ukabila na ubaguzi." Anne Rwigara amesema kuwa family yake imewekwa kizuizini.
Vyombo vya serikali nchini Rwanda vilimuondoa Diane Rwigara katika mbio za uchaguzi wa Agosti kwa madai ya kuwa alikuwa hana sifa, hivyo kumfanya Rais Paul Kagame kushinda kwa urahisi.
Serikali ya Kagame inatuhumiwa na makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu kwamba inawatishia wapinzani.

No comments:

Post a Comment