Wanafunzi watano na mlinzi wa usiku wamepigwa risasi na kuuwawa mapema Jumamosi asubuhi katika shule ya mseto ya Lokichogio huko kaunti ya Turkana, Kenya.
Mkuu wa polisi wa kaunti hiyo Kamishna Seif Matata amethibitisha kuwa mmoja wa washambuliaji hao alikuwa ni mwanafunzi katika shule hiyo ambaye alikuwa amesimamishwa kwa muda kuendelea na masomo.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Kenya shambulizi hilo la silaha ya moto liliotokea kati ya saa tisa na nusu na kumi alfajiri Jumamosi.
“Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa katika tukio hilo. Hatuwezi kuthibitisha idadi kamili mpaka tutakapo wasiliana na uongozi wa hospitali,” amesema Matata.
Shule hiyo iko umbali wa kilomita 200 kutoka mpaka unaogawanya Kenya na
Sudan Kusini.
Sudan Kusini.
No comments:
Post a Comment