Katika kilele cha siku ya mtoto wa kike duniani, kilichoadhimishwa wiki hii jumla ya mangariba 63 Tanzania wamechukua uamuzi wa kuacha kazi ya ukeketaji wa watoto wa kike.
Badala yake watu hao wameanza kujifunza ujasiriamali utakaowasaidia kujiongezea kipato.
Shirika la Kutokomeza ukeketaji Tanzania limeweza kuwaelimisha wasichana 2,166 kuhusu madhara ya ukeketaji na kuweza kuepushwa katika vitendo hivyo ambavyo ni vya kikatili na kinyume cha sheria.
Vyanzo vya habari vimeripoti zaidi kuwa elimu thabiti ya athari za ukeketaji iliyowafikia wakeketaji hao iliwafanya waamuwe kuacha na kuanza kufanya shughuli nyingine ikiwemo za ujasiriamali wa bidhaa mbalimbali zitakazosaidia kujikimu kimaisha.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Charles Mlingwa alisema mkoa huo umeweza kupunguza vitendo vya ukatili kwa watoto kwa kiwango kikubwa kuanzia asilimia 70 hadi 37 iliyopo sasa.
No comments:
Post a Comment