Thursday, October 19

Lulu kupanda kizimbani kwa mauaji ya Kanumba

Dar es Salaam. Msanii wa kike wa fani ya uigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael, maarufu Lulu amewasili Mahakama Kuu anakokabiliwa na kesi ya mauaji ya bila kukusudia.
Lulu ambaye yuko nje kwa dhamana anadaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia kinyume cha kifungu cha 195 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu.
Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7,2012 nyumbani kwa Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Kesi inasikilizwa na Jaji Sam Rumanyika.

No comments:

Post a Comment