Saturday, October 21

Kuiombea Somalia: Ni kwa nini ulimwengu uliisahau Mogadishu?

Wasomalia wenyewe wamekuwa wakitumia uwezo wa mitandao ya kijamii kuchangisha misaada.Haki miliki ya pichaUCL BME NETWORK/UNION UCL
Image captionWasomalia wenyewe wamekuwa wakitumia uwezo wa mitandao ya kijamii kuchangisha misaada.
Ni kipi hutokea kwenye mitandao ya kijamii baada ya shambulizi la kigaidi? Vitambulisha mada busambaa ambayo huitisha maombi. Watumiaji wa mitandao mara nyingi husambaza picha za uharibifu na watu kuonyesha husuni.
Lakini baada ya shambulizi baya siku ya Jumamosi mjini Mogadishu ambalo liliwaua watu 281, baadhi ya mitandao ya kijamii wamekuwa wakiuliza ni wapi uzalendo kwa Somalia, na mbona hakuna hashi tagi sawa na za wakati wa mashambulizi nchini Marekana na Ulaya.
Shambulizi la lori la simu ya Jumamosi lilikuwa baya zaidi la kigaidi kuwai kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati za mwaka 2007. Miili mingine ilichomeka hadi kiwango cha kutotambuliwa.
Kati ya wale waliotambuliwa, mmoja wa waathiriwa alikuwa Maryan Abdullahi, mwanafunzi anayesomea udaktari ambaye alitarajia kufuzu siku iliyofuatia.
Baba yake alikuwa amesafiri kwenda mjini Mogadishu kuhudhuria shereha za kufuzu kwake lakini badala yake akahudhuria maziko yake.
Maryam Abdullahi has been identified as one of the 267 people killedHaki miliki ya pichaANFA'A ABDULLAHI
Image captionMaryam Abdullahi ni mmoja wa watu 267 waliouawa
Hadithi kama hizi za kuvunja moyo si hazifanani na zile ambazo husambaa wakati wa mashambulizi na majanga ya kiasili kote duniani wakati watu hupoteza maisha.
Kati ya siku ya Jumamosi wakati shambulizi hilo lilitokea na mapema Jumatatu kitambulisha mada #IAmMogadishu ilikuwa na Twitter 200 na zaidi, lakini ilipotimia Jumanne kulikuwa na zaidi ya Twitter 13,000 wakati watumiaji wa mitandao ya kijamii walielezea hisia zao baada ya vyombo vya hahari kutoangazia mashambulizi hayo.
Makumbusho kadha yameandaliwa na jamii za wasomalia kote Uingerezea na Marekani yakiwemo ya siku ya Jumanne ya Kings College London's Somali society.
"Kwa sababu ya ukosefu wa uzalendo kwa Somalia, tunataka kuonyesha kuwa kuna watu walio wazalendo kwa Somalia," alisema muandalizi mmoja.
Licha ya kutokepo uzalendo wa nchi za magharibi katika mitandao ya kijamii, Wasomalia wenyewe wamekuwa wakitumia uwezo wa mitandao ya kijamii kuchangisha misaada.
Mitandao ya kijamii ni maarufu nchini SomaliaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMitandao ya kijamii ni maarufu nchini Somalia

No comments:

Post a Comment