Saturday, October 21

Doris Wanjira: Ni wajibu wangu kulinda wanawake wakitumia matatu Kenya

Picha ya hivi karibuni ya Doris Wanjira akiwa amembeba mtoto ilisambaa sana mtandaoni
Image captionPicha ya hivi karibuni ya Doris Wanjira akiwa amembeba mtoto ilisambaa sana mtandaoni
Magari ya uchukuzi wa umma katika miji mingi duniani yamekuwa hatari kwa wanawake. Visa vya udhalilishaji wa kimapenzi pamoja na udhalilishaji wa aina nyingine vimekuwa vikiripotiwa.
Maeneo mbalimbali duniani, watu wamejaribu kutafuta suluhu.
Nchini Kenya, Doris Muthoni Wanjira, 38, ni utingo kwenye gari la uchukuzi maarufu kama matatu.
Ameambia waandishi wa makala za msimu wa Wanawake 100 wa BBC kwamba wanawake hukabiliwa na changamoto na hatari zaidi katika magari ya umma kuliko wanaume, hata katika kuajiriwa.
"Ni vigumu kupata gari la kufanyia kazi iwapo wewe ni mwanamke. Wanawake hufanya bidii tuseme mara tatu zaidi ndipo wapate kazi.
"Abiria na madereva (wa kike) katika magari ya matatu hupitia mengi: kudhalilishwa kimapenzi, na wengi kudhaniwa kuwa ni makahaba.
"Kwa utingo, baadhi (ya abiria wa kiume) huenda hatua zaidi ya hata kukataa kulipa nauli na tunapowakabili huwa wanatutusi kwa maneno na wakati mwingine hata kutushambulia."
Doris anasema changamoto hizo hata hivyo hazijamzuia kufanya kazi yake, na anahisi kwamba ni jukumu na wajibu wake kuwalinda wanawake katika magari ya uchukuzi wa umma.
"Nafikiri ni muhimu kwamba tuonekane tukifanya kazi za aina hii, inawapa wanawake wengine matumaini kwamba wanaweza kufanya kazi hii sawa na wanaume.
"Na kusema kweli, wanawake ni madereva wazuri kuliko wanaume.
Anita Nderu: Nilishtukia mkono wa mwanamume kwenye ziwa langu
"Huwa twaendesha magari kwa mwendo wa polepole lakini bado huwa twatimiza malengo ya siku na abiria wengi wa kike sasa wanatumia magari yetu kwa sababu tunajua jinsi ya kuifanya rahisi kwao kupanda au kushuka na huwa twawahudumia kwa heshima."

No comments:

Post a Comment