Saturday, October 21

Kifungo cha waliokamatwa wakibusu chadumishwa na mahakama Tunisia

Kifungo cha waliokamatwa wakibusu chadumishwa na mahakama TunisiaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKifungo cha waliokamatwa wakibusu chadumishwa na mahakama Tunisia
Mahakama ya rufaa nchini Tunisia imedumisha hukumu ya wapenzi wawili waliokamatwa mwezi Septemba kwa kubusu wakiwa ndani ya gari lao.
Nessim Ouadi, ambaye ni raia wa Ufaransa pia alilaumiwa kwa kupuuza maagizo ya baada ya kukamatwa pamoja na mpenzi mwanamke raia wa Tunisia.
Wawili hao walipewa vifungo vidogo ikiwa ni miezi minne kwa mwanamume na miwili kwa mwanamke tofauti na walivyopewa mwezi Oktoba.
Kesi hiyo ilisababisha malalamiko katika mitandao ya kijamii na kuzua mjadala nchini Tunisia kuhusu maadili katika maeneo ya umma na wajibu wa polisi.
Mkuu wa mshataka alisema kuwa kesi hiyo imeripotiwa kwa njia isiyofaa na vyombo vya habari vya kimataifa na kuwa wawili walikuwa uchi na walikuwa wakifanya mapenzi wakati walisimamishwa na polisi.

No comments:

Post a Comment