Saturday, October 21

Blac Chyna aishtaki familia ya Kardashian

Blac Chyna ameishtaki familia ya The Kardashian kwa madai kwamba ndio iliosababisha kufutiliwa mbali kwa kipindi chake cha RuningaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBlac Chyna ameishtaki familia ya The Kardashian kwa madai kwamba ndio iliosababisha kufutiliwa mbali kwa kipindi chake cha Runinga
Blac Chyna anaishtaki familia ya The Kardashian kwa madai kwamba ndio iliosababisha kufutiliwa mbali kwa kipindi chake cha Runinga.
Anadai kwamba familia hiyo inataka kumharibia.
Wakili wa Blac Chyna aliithibitishia BBC kwamba Kris Jenner ametajwa kama mtetezi katika kesi hiyo pamoja na Kourtney, Kim na Khloe Kardashian mbali na Kendall na Kylie Jenner.
Mwakilishi wa familia hiyo hajatoa tamko lolote kufuatia ombi hilo la BBC.
Kesi hiyo inajiri baada ya Uhusiano kati ya mlalamishi huyo na Rob Kardashian kugonga mwamba , wakati ambapo walikuwa wamepata mtoto wa kike.
Black Chyna mwenye umri wa miaka 29 anadai alipigwa na kunyanyaswa na aliyekuwa mchumba wake Rob Kardashian.
Rob Kardashian na mpenziwe wa zamani Blac ChynaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRob Kardashian na mpenziwe wa zamani Blac Chyna
Nakala za mahakama dhidi ya familia hiyo na kuchapishwa kamili na chombo cha habari cha Buzzfeed zinadai kwamba Rob Kardashian ni myanyanyasaji na anataka kumharibia Angela White {Blac Chyna}.
Chombo hicho cha habari pia kinaishutumu familia hiyo kwa kutumia umaarufu wao, utajiri na uwezo kulipiza kisasi na kuzuia kuanzishwa kwa kipindi chake cha runinga Rob na China kwa msururu wa pili.
Hatua hiyo inajiri wiki mbili baada ya Rob Kardashian kuwasilisha kesi mahakamani akisema kuwa ni yeye ndiye aliyemshambulia, madai ambayo blac Chyna amekana.

No comments:

Post a Comment