Maafisa nchini Misri wanasema kuwa takiban maafisa 53 wa usalama na wapiganaji wa kiislam kumi na watano wameuawa katika makabiliano yaliyotokea katika eneo la jangwa magharibi mwa nchi hiyo .
Wizara ya mambo ya ndani nchini humo inasema kuwa wapiganaji waliwafyatulia risasi wanajeshi wakati walipokuwa wakifanya uvamizi kwenye maficho yao, karibu na eneo lenye chemi chemi Bahariya .
Duru za usalama zinasema kuwa wapiganaji walikuwa na uelewa zaidi wa eneo hilo na afisa wa kijeshi aliyetoa maagizo ya uvamizi alishindwa kuagiza wanajeshi kuimarisha kikosi chake .
Taarifa moja inasema kuwa wapiganaji hao ni wajumbe wa kikundi kinachofahamika kama Hasm, ambacho kiliwahi kuyashambulia majeshi ya usalama awali.
No comments:
Post a Comment