Mwanamke wa umri wa makamo amefariki kutokana na Kimbunga Ophelia katika Visiwa vya Uingereza.
Tawi la mti liliangukia gari la mwanamke huyo eneo la Waterford Magharibi. Abriia mwingine aliyekuwa kwenye gari hilo alijeruhiwa huku upepo mkali uliotokana na kimbunga hicho ukiendelea kupiga Jamhuri ya Ireland.
Nyumba 120,000 zimeachwa bila umeme katika Jamhuri ya Ireland, ambapo serikali imelituma jeshi kusaidia juhudi za uokoaji.
Tahadhari imetolewa Ireland Kaskazini, Wales, kusini magharibi mwa Scotland na Isle of Man hadi usiku.
Upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita 176 kwa sasa umekuwa ukipiga ppwani ya kusini mwa Ireland.
Kumetolewa tahadhari pia maeneo ya Scotland, kaskazini mwa England na Wales kwamba kunaweza kuwa na "upepo mkali".
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ameahirisha ziara yake Belfast kutokana na kimbunga hicho.
Ophelia sasa kimeorodheshwa kuwa kimbunga cha ngazi ya kwanza na Kituo cha Taifa cha Vimbunga cha Marekani.
No comments:
Post a Comment