Monday, October 16

Cairo jiji hatari zaidi kwa wanawake duniani

Mji wa Cairo una wakazi 22.8 milioniHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMji wa Cairo una wakazi 22.8 milioni
Jiji la Cairo ndilo hatari zaidi kwa wanawake kuishi duniani miongoni mwa majiji duniani, utafiti wa shirika la Thomson Reuters Foundation unaonesha.
London nao ndio mji bora zaidi kwa wanawake kuishi.
Mji wa Kishasha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unafuata Cairo, nao mji wa Lagos nchini Nigeria ni wa nane kwenye orodha hiyo.
Jumla ya majiji 19 makubwa yalichunguzwa - ambayo ni majiji yenye idadi ya watu inayofika milioni kumi na zaidi.
Miongoni mwa yaliyozingatiwa kwenye utafiti huo ni unyanyasaji wa kingono, utamaduni unaowadhalilisha wanawake pamoja na upatikanaji wa huduma bora ya afya kwa wanawake, fedha na elimu.
Wataalamu katika haki za wanawake waliombwa ushauri wao wakati wa kufanywa kwa utafiti hao, miongoni mwao akiwa mwanahabari Shahira Amin, ambaye aliambia Thomson Reuters:
"Mambo yote kuhusu wanawake katika jiji hilo ni hatari. Hata kutembea tu barabarani, na hunyanyaswa sana, kwa maneno na kwa vitendo."

No comments:

Post a Comment