Timu ya wataalamu kutoka Jukwaa la Haki Jinai nchini ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome inatembelea Magereza katika mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma ili kujionea changamoto zinazowakabili wafungwa na mahabusu nchini katika kupata haki zao wakiwa vizuizini au magerezani na kuangalia namna ya kuzitatua.
Akizungumza katika siku ya kwanza ya ziara hiyo mjini Iringa, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Mchome amesema utekelezaji wa mradi huo pia unalenga kuziongezea uwezo taasisi zinazoshughulika na utoaji haki na kusimamia haki za binadamu nchini ili ziweze kutoa huduma stahiki kwa watanzania ya utoaji haki na ulinzi wa haki za binadamu.
Amesema ni matarajio ya Serikali kuwa ziara hiyo itawezesha taasisi zinazosimamia utoaji haki nchini kuchukua hatua katika kuhakikisha wafungwa na mahabusu wanapata haki zao kwa wakati.
Ujumbe huo wa jukwaa la haki jinai unamshirikisha Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) Biswalo Mganga, Naibu Mkurugenzi Upelelezi Makosa ya Jinai nchini (DDCI) Charles Kenyela, Ofisi ya Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Magereza na Jeshi Polisi.
Ujumbe huo umetembelea Gereza la wilaya ya Iringa, Selo iliyoko katika kituo cha Polisi Iringa mjini, Gereza la Wilaya Njombe na selo iliyoko katika kituo cha Polisi Njombe na kujionea mazingira yaliyopo na kusikiliza kero zinazowakabili wafungwa na mahabusu walioko katika vituo hivyo vya polisi na magereza hayo katika kupata haki zao.
Wananchi hao waliomba kupata msaada katika maeneo ya kufikishwa mahakamani kwa wakati, uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili kufanywa kwa wakati, kupatiwa nakala za hukumu kwa wakati ili wawahi muda wa kukata rufaa na mashitaka yao kusikilizwa kwa wakati ikiwa ni pamoja na kusikilizwa kwa rufaa zao.
Ziara hiyo ni utekelezaji wa mradi wa upatikanaji haki na ulinzi wa haki za binadamu nchini unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa –UNDP.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka akiongea na wataalamu wa Jukwaa la haki jinai nchini ambao walioongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome walipoanza ziara ya kutembelea magereza na vituo vya polisi mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza akiwakaribisha ofisini kwake wataalamu wa Jukwaa la
haki jinai nchini ambao walioongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome mjini Iringa walipoanza ziara ya kutembelea magereza na vituo vya polisi mkoani humo juzi.
Wataalamu kutoka taasisi zinazosimamia utoaji haki nhini ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome wa pili kulia waliosimama mbele wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka wapili kushoto waliosimama mbele Wataalamu hao walikwenda kumsalimia Mkuu wa Mkoa wa Njombe kabla ya na kutembelea gereza la wilaya ya Njombe na kituo cha Polisi cha wilaya hiyo na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko kizuizini katika maeneo yao na kutatua changamoto zinazowakabili.
Timu ya wataalamu kutoka Jukwaa la Haki Jinai nchini ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. SifuniMchome katika picha ya pamoja na askari magereza nje ya gereza la wilaya ya njombe baada ya kutembelea gereza hilo na kuzaungumza na wafungwa na mahabusu walioko katika gereza hilo mjini Njombe jana
ilikujionea changamoto zinazowakabili wafungwa na mahabusu nchini katika kupata haki zao wakiwa vizuizini au magerezani na kuangalia namna ya kuzitatua.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza (katikati waliosimama mbele) katika picha ya poamoja na wataalamu wa Jukwaa la haki jinai nchini ambao walioongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome baada ya kutoka kumsalimia Mkuu huyo wa mkoa Ofisini kwake mjini Iringa walipoanza ziara ya kutembelea magereza na vituo vya polisi mkoani humo juzi.
No comments:
Post a Comment