Tuesday, October 17

SERIKALI YA OMAN KULIKARABATI JUMBA LA AJABU AKA BEIT EL AJAIB ZANZIBAR

Na Salum Vuai, MAELEZO
 UJUMBE wa Serikali ya Oman uliokuwepo Zanzibar tangu Oktoba 12, 2017, leo umebariki maandalizi ya matengenezo makubwa ya jengo la kihistoria Beit El Ajaib lilioko Forodhani katika
Mji Mkongwe wa Zanzibar. 
Ujumbe huo ukiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dk. Mohammed Hamad Al Rumhy, umelitembelea jengo hilo ukiambatana na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukagua hali yake halisi. 
 Lengo la ziara hiyo lilikuwa kuweka jiwe la msingi kama ishara ya maandalizi ya matengenezo hayo chini ya ufadhili wa Serikali ya Oman inayoongozwa na Sultan Qaboos bin Said, yanayotarajiwa kuanza wakati wowote kutokea sasa. Jengo la Beit El Ajaib lililojengwa mwaka 1883 wakati wa utawala wa Sultan wa pili wa Zanzibar Barghash bin Said, limeachwa kutumika kwa miaka kadhaa sasa kutokana na kukabiliwa na uchakavu mkubwa ikiwemo kuanguka baadhi ya kuta zake. 
Beit El Ajaib ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii hapa Zanzibar, na kabla kuzuiwa matumizi yake, lilikuwa likiingizia mapato serikali kwa kutembelewa na watalii wengi kutoka nchi mbalimbali duniani. 
Matengenezo hayo yanatarajiwa kulijejeshea haiba jengo hilo ambalo ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii humu visiwani, na kuanza kutumiwa tena wa shughuli za kitalii. OKTOBA 2017

Jumba la Ajabu aka Beit El Ajaib Zanzibar  

Jumba la Ajabu aka Beit El Ajaib linavyoonekana kwa sasa

No comments:

Post a Comment