Monday, October 2

Catalonia 'yapata haki ya kuwa huru'

Crowds gather to await the result of the Independence referendum at the Placa de Catalunya on October 1, 2017 in BarcelonaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionCatalonia 'yapata haki ya kuwa huru'
Kiongozi wa eneo la Catalonia Carles Puigdemont anasema kuwa eneo la Uhispania limepata haki ya kuwa huru kufuatia kura ya maoni yenye utata ambayo imekubwa na ghasia.
Alisema kuwa sasa mlango umefunguliwa kwa eneo hilo kutangazwa kuwa huru.
Maafisa wa Catalonia baadaye walisema kuwa asilimia 90 ya wale walioapiga kura waliunga mkono uhuru kwenye kura ya maoni ya siku ya Jumapili.
Mahakama ya katiba nchini Uhispania imeitangaza kuta hiyo ya maoni kuwa iliyo kinyume na sheria na mamia ya watu walijeruhiwa wakati polisi walitumia nguvu kujaribu kuzuia zoezi hilo.
Image captionKiongozi wa neo la Catalonia Carles Puigdemont anasema kuwa eneo la Uhispania limepata haki ya kuwa huru
Polisi walichukua makaratasi ya kupigia kura na masanduku kutoka kwa vituo vya kupigia kura.
"Siku hii ya leo ya matumaini na mateso, watu wa Catalonia wameshinda haki yao ya kuwa na taifa huru kama jamhuri," Bw Puigdemont alisema alipotoa hotuba kupitia televisheni akiandamana na maafisa wengine wa vyeo vya juu wa Catalonia.
"Serikali yangu kwa muda wa siku chache zinazokuja itatuma matokeo ya kur ya leo kwemda kwa bunge la Catalonia, ili ifanye kuambatana na sheria ya kura ya maoni."
Image captionMwanamke huyu alipata jereha la kichwa huko Barcelona

No comments:

Post a Comment