Ni kauli ya Hadija Aziz Ali, baada ya kusikia taarifa kwamba ameongoza mtihani wa darasa la saba kitaifa.
Hadija ni miongoni mwa wanafunzi 41 wa Shule ya Msingi Sir John ya jijini Tanga waliofanya mtihani wa kitaifa wa darasa la saba mwaka huu.
Kwa matokeo yaliyotolewa leo Ijumaa Oktoba 20,2017 na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Hadija ameongoza kitaifa na kuiwezesha shule yake kushika nafasi ya nne kitaifa na kuongoza katika wilaya na Mkoa wa Tanga.
Hadija amesema aliingia chumba cha mtihani akiwa na nia ya kutimiza ndoto zake za kufaulu ili apate nafasi ya kusoma masomo ya juu na hatimaye awe daktari bingwa wa magonjwa ya watoto baadaye.
Akizungumza akiwa nyumbani kwao mtaa wa Donge jijini Tanga, Hadija amesema siri ya kufanya vizuri ilitokana na juhudi za walimu wake, ushirikiano baina ya wanafunzi na wazazi ambao walikuwa kila siku wakimpa moyo.
“Nawashukuru wanafunzi wenzangu Florence Julius, Saada Ahmed na Lina John, nitawakumbuka siku zote kwa sababu tulikuwa tukipeana moyo tukiwa
darasani,” amesema Hadija.
Mama yake amwaga chozi
Jane Kihiyo (48), mama mzazi wa Hadija akizungumza huku akilia kwa kutoamini matokeo hayo, amesema mwanaye alitambua kwamba atafaulu kwa sababu alikataa kufanya mitihani ya kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za binafsi.
“Mwanangu alikataa kabisa kufanya interview kwenye shule za sekondari za binafsi, mimi na baba yake tulihangaika kutafuta shule nzuri lakini alikataa katakata,” Kihiyo ambaye ni muuguzi katika
kituo cha afya cha Besha jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment