Thursday, September 21

WATU WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA PWANI BAADA YA KUKAMATWA NA GUNIA NANE ZA BHANGI


 JESHI la Polisi  Mkoa wa Pwani  wamewakamata watuhumiwa wawili  ambao wameshikwa  wakisafirisha  dawa za kulevya  aina ya Bhangi  magunia nane.
 Watuhumiwa hao walionaswa  na Jeshi la Polisi wamefahamika  kwa  mjina Abraham Michael  mwenye umri wa miaka  31 mkaazi wa Jijini Dar es Salaam na Godfrey  Malakasuka  mwenye umri wa miaka 21 mkaazi wa Kimara  waliokamatwa katika eneo la Ubena Zomozi wakitokea Mkoani Morogoro kuelekea Jijini Dar es Salamaa.
Akizungumza na  waandishi wa habari  Kamanda wa Mkoa wa Pwani ACP Jonathan Shanna  alisema kuwa watuhumiwa  wamekamatwa na vidhibiti  hivyo wanastahili  kupata adhabu kali pindi watakapofikishwa  mahakamani

No comments:

Post a Comment