Kikao cha wataalamu wa masuala ya teknolojia ya Mawasiliano leo kimeendelea mjini Bagamoyo kwa kuhusisha Wadau wakuu katika masuala ya utoaji huduma nchini zikiwemo Wizara, Taasisi , Mashirika na Makampuni binafsi.
Katika kikao cha leo wadau wanajadili mapendekezo ya timu ya wataalamu iliyokutana siku ya kwanza ya kikao hicho kuhusu kuundwa kwa timu ya pamoja ya wataalamu ambayo itapendekeza mfumo rafiki na rahisi utakaorahisisha utoaji huduma nchini na kuboresha maisha ya watanzania kwa kutumia mfumo wa Taifa wa Utambuzi na Usajili wa watu unaosimamiwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Akichangia katika siku ya pili ya mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Balozi Hassan Yahya Simba amesema ubora wa huduma na maendeleo ya Taifa unategemea uwepo wa mfumo huu ambao ni kwa manufaa si tu ya Serikali lakini pia kwa Sekta binafsi.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia (World Bank) Ndugu Robert Polacious akizungumza kwenye siku ya pili ya kikao cha wadau kuhusu kuundwa kwa mfumo wa kidigitali utakaoungalisha mifumo ya taarifa nchini kwa kutumia Mfumo Mama wa Utambuzi na Usajili wa Watu unaosimamiwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NDIA)
Dr. Elias Mturi mtaalamu katika teknolojia ya mawasiliano akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya Wadau Bagamoyo.
Amesema kwa sasa Serikali ina kila sababu ya kuwa na mfumo huu kutokana na mahitaji yaliyopo katika kuboresha huduma za Kijamii, kuwezesha wananchi kushiriki kupata huduma za kifedha na Kibenki, kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato, uchaguzi na kuongeza fursa za uzalishaji katika kufikia maendeleo ya haraka.
Washiriki wengine wanaoshiriki kuchangia kuundwa kwa mfumo huu ni Kampuni za simu Tanzania, Benki, Mashiriki ya Kimataifa yanayotoa huduma nchini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Wataalamu wa ndani na nje katika masuala ya teknolojia na wakuu wa Taasisi wa nchi za Estonia na India ambazo tayari mfumo wa kuunganisha taarifa kidigitali (Digital ID ecosystem) imeshaanzishwa na kupata mafanikio makubwa.
Warsha hii inategemewa kumalizika na maazimio ya pamoja ya namna mfumo huo utakavyoundwa nchini kwa kutumia teknolojia na kushiriki wadau wote muhimu.
Wawakilishi wa Umoja wa Makampuni ya Simu Tanzania wakiwasilisha mada na maoni ya wadau katika kuundwa kwa mfumo wa Taifa wa kidigitali unaounganisha mifumo ya taarifa kupitia mfumo Mama wa Utambuzi na Usajili wa Watu unaomilikiwa na NIDA. Katikati ni ndugu Paul Bomani wa AIM Group akiwasilisha mada kwa niaba ya MOAT.
Washiriki wa Warsha ya wataalamu na wadau wakijadiliana kwenye vikundi wakati warsha ya kuunda mfumo wa kidigitali wa mawasiliano Tanzania inayofanyika Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment