Friday, September 15

Waliokamatwa na mzigo wa almasi JNIA wafikishwa Kisutu

Shehena ya Almasi iliokamatwa katika Uwanja wa
Shehena ya Almasi iliokamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  hivi karibuni. Ambayo jana  ilioyeshwa hadharani wakati Waziri wa  Fedha na Mipango, Dk  Philip Mpango na viongozi wegine wa Serikali,   alipokwenda kukabidhiwa ripoti  ya uchunguzi kuhusu  utoroshwaji wa madini hayo kiwanjani hapo jana. Picha na Ikulu 
Dar es alaam. Watuhumiwa waliokamatwa na mzigo wa almasizenye thamani ya Sh 32.3 bilioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA), wamefikishwa mahakamani Kisutu asubuhi leo Ijumaa.
Watuhumiwa hao walikamatwa na mzigo huo ambao ulizuliwa na Serikali ili ufanyiwe tathimini upya kujua thamani halisi baada ya thamani iliyotumika kutiliwa mashaka na Serikali.
Jeshi la polisi liliwashikilia watuhumiwa wanne kwa uchunguzi na hatua nyingine za kisheria baada ya kuzuia mzigo huo.
Mzigo huo wa almasi ulikuwa unatoka mgodi wa Mwadui ambao ni wa ubia kati ya Serikali na kampuni ya Petra Diamonds ya Afrika Kusini kwa hisa 25 za Serikali na Petra  Diamonds hisa 75.

No comments:

Post a Comment